Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeMusicRoseline: Ingizo jipya la Dancehall Bongo
| + -

Roseline: Ingizo jipya la Dancehall Bongo

Monday, 25 June 2012 05:52 Deiwaka World News - Music
Print PDF

Roseline: Ingizo jipya la Dancehall Bongo

Roseline Muhagachi, ni kifaa kipya kwenye ulimwengu wa Dancehall na Bongo Fleva kwa jumla.

Ameanza kuthibitisha ndani ya muda mfupi kwamba ni moto wa kuotea mbali, kwani anafanya vema kwa sasa.

Unabisha? Tupia macho kwenye runinga Bongo, angalia vipindi vya muziki, utaona video ya wimbo Bumchaka Chaka, inavyogongwa na kupigiwa saluti na mashabiki. Audio pia inafanya vizuri, kuonesha kuwa kazi ni imeshakubalika.

Je, Roseline atakomaa kimuziki au atapotea kama dada zake wengine ambao walitamngulia? Swali hilo analijibu moja kwa  moja: “Naamini nitakuwepo sana sokoni. Kazi nzuri zaidi zinakuja, Bumcha Chaka ambao nimemshirikisha Country Boy ni utangulizi tu.”

Kwa sasa, mbali na muziki Roseline ni mwanafunzi mwaka wa pili kwenye Chuo cha Ustawi wa Jamii, akisomea shahada ya Huduma za Jamii (Social Work).