Baada ya kutengana na mume, Uwoya ni aibu
Maisha ya mwigizaji staa wa sinema za Bongo, Irene Uwoya bila kuwa na mumewe, Hamad Ndikumana 'Katauti' yanaonekana kuwa ya aibu tupu kufuatia siku za karibuni kubadilika tabia, hasa kwenye eneo la kujiheshimu.
Marafiki wa staa huyo wamepasha kuwa Uwoya amekuwa akitenda mambo mengi ya aibu kwa sababu ameshatengana na mumewe ambaye kwa sasa amerudi kwao, Rwanda.



“Yaani Uwoya sasa hivi hana tofauti na msichana ambaye hafikirii kuolewa, amechangamka kila idara, hajali cha ndoa wala mume, anaonekana anajipongeza kwa ndoa yake kuvunjika,” alisema rafiki wa karibu wa Uwoya.
Tabia nyingine ambayo imegundulika kuwa staa huyo anayo kwa sasa ni kujiachia na waume za watu pamoja na waigizaji wenzake wa kiume huku ikidaiwa hachagui mahala popote yeye ni ‘kambi’.
“Siku hizi Uwoya anaweza kukaa sehemu, akamuegemea mwanaume ambaye ni mume wa mtu au akamfanyia msanii mwenzake vitendo ambavyo kwa mtu kama yeye aliye kwenye ndoa hatakiwi kuvifanya, hata kama ndoa yenyewe ilivunjika,” aliendelea kuanika rafiki huyo.
Akaendelea: “Lakini bwana hata hao wanaume wenyewe wangekuwa wanaangalia; ya nini kuchezeana na msanii ambaye siku ikifika, mkatoka magazetini mnapiga kelele kulalamika?”
Rafiki huyo akaongeza: “Mabadiliko mengine ambayo Uwoya anaonekana kuwa nayo ni mavazi ambapo inadaiwa licha ya kuzoeleka kwa kuvaa mavazi ya nusu utupu akiwa na mumewe lakini kwa sasa amezidisha, anaweza kuvaa kigauni kifupi hadi akikaa nguo ya ndani inaonekana.”
Mbali na mavazi, kujiachia na wanaume hadharani, imebainika kuwa, kwa sasa mwigizaji huyo ndiye anayeongozwa kwa kutetwa na marafiki zake wa karibu, wengi wakionesha kutomuunga mkono kufuatia kitendo chake cha kukubali ndoa yake ivunjike.
Hilo lilionekana hivi karibuni alipotinga kwenye Hotel Hyatt Kilimanjaro Kempinski, jijini Dar es Salaam ambapo staa mwenzake, Wema Sepetu alikuwa akizindua filamu ya Superstar.
Uwoya alitinga ukumbini akiwa amevaa vazi jeusi na la ajabu, chini alivaa soksi nyeusi tu bila viatu huku kucha za vidole vya mikononi zikiwa ndefu na kupakwa rangi nyekundu hivyo kuonekana kama mtu wa kwenye filamu za kutisha.
“Hivi Irene amevaaje leo jamani? Ina maana kutoka moyoni ameona vile ni sawa?” alisikika akihoji mmoja wa mastaa wa kike Bongo.