Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeSport
| + -

Sports News

Wednesday, 25 July 2012 05:26 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Simba out Kagame, yapigwa 3-1 na Azam

Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, leo imetolewa katika michuano ya Kombe la Kagame baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Azam FC katika mechi ya robo fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji John Bocco ndiye aliyeibuka shujaa wa Azam baada ya kuifungia mabao yote matatu, moja kipindi cha kwanza na mengine kipindi cha pili. Bao pekee la Simba lilifungwa na Shomari Kapombe.

Ushindi huo umeiwezesha Azam kutinga nusu fainali, ambapo sasa itakutana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Vita imefuzu kucheza hatua hiyo baada ya kuitoa Atletico ya Burundi mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa kuanzia saa nane mchana.

Mechi nyingine ya nusu fainali itazikutanisha Yanga na APR ya Rwanda.

Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa Mafunzo ya Zanzibar kwa penati 5-3 wakati APR iliitoa URA ya Uganda kwa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa ratiba, mechi zote mbili za nusu fainali zitachezwa Alhamisi wiki hii. Mechi ya kwanza itazikutanisha Azam na AS Vita wakati katika mechi ya pili, Yanga itavaana na APR.

Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Jumapili, ikitanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.

 
Monday, 16 July 2012 10:10 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Manji ashinda uenyekiti Yanga

Mfadhili wa zamani wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji, ameshinda uenyekiti wa klabu hiyo, katika uchaguzi mdogo, uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Yanga ilifanya uchaguzi jana kuziba nafasi za viongozi wa klabu hiyo, walioachia ngazi kwa kujiuzulu kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Waliojiuzulu ni aliyekuwa mwenyekiti, Lloyd Nchunga, Makamu Mwenyekiti, Davies Mosha pamoja na wajumbe mbalimbali.

Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mshindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.

Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama  wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya  Utendaji.

Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.

Matokeo kamili ya wagombea ni:


Nafasi ya Mwenyekiti:

Yusuf Manji (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%


Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:

Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%


Nafasi ya Ujumbe:

Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)


kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni

Mwenyekiti: Yusuf Manji,

Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga

Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama

 

 
Monday, 09 July 2012 05:38 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Wabunge Simba waitoa nishai Yanga

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana walikipiga katika mechi ya soka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mashabiki wa Simba kuwatoa nishai wenzao wa Yanga.

Mechi ilikuwa kali lakini mpaka mwisho wa mchezo, matokeo yalikuwa 0-0, hivyo kulazimika mshindi apatikane kwa mikwaju ya penalti.

Katika mikwaju ya penalti, Simba iliibuka na ushindi wa matuta 3-2.

 
Monday, 09 July 2012 05:27 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Cheka amkimbia Kaseba ulingoni

Bondia Francis Cheka, jana alithibitisha kuwa yeye hafai kuwa bingwa tena baada ya kumkimbia Japhet Kaseba ulingoni.

Wakati pambano lilipotajwa, Cheka alipanda ulingoni na kitu cha kushangaza watu, alikataa kupigana kwa kile kilichoonekana ni kumuogopa Kaseba.

Baada ya kukacha ulingoni, baadhi ya watu wa karibu na Cheka walisema kuwa bondia huyo amekuwa hafanyi mazoezi ya kutosha, hivyo aliogopa kupigwa.

“Cheka amekuwa mzembe siku hizi, nadhani kalewa sifa. Alijua atapigwa na Kaseba, hilo sisi watu wa karibu tunajua na alituambia,” alisema rafiki wa Cheka.

 
Monday, 09 July 2012 05:02 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Wema, Wolper watoka droo

Mastaa Wema Sepetu na Jacqueline Wolper ambao walichapana jana kumaliza ubishi wa nani mbabe kati yao, pambano lao liliisha pasipo mshindi kupatikana.

Waamuzi waliochezesha pambano hilo, walisema kuwa mastaa hao wametoka droo baada ya kulingana pointi.

Pengine Wolper angeweza kushinda pambano hilo kwa sababu alikuwa anashambulia mara nyingi lakini mpaka mwisho hakuweza kurusha ngumi hata moja.

Baada ya mpambano huo, mastaa hao walikumbatiana kuonesha kuwa hawakuwa na bifu ila ni mchezo tu.

 
Friday, 06 July 2012 14:47 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Kaseba, Cheka wapima tayari kwa pambano

Mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba, leo wamepima uzito tayari kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kaseba na Cheka, watapigana kwenye pambano la raundi nane, katika tamasha la Usiku wa Tumaini ambalo litafanyika kuanzia kesho na kumalizika siku inayofuata.

Baada ya kupima, kila mmoja ametamba atampiga mwenzake.

Kaseba alisema: “Huu ndiyo mwisho wa Cheka kutamba, mara ya mwisho tulipopigana, shabiki aliingilia kati na Cheka akapwa ushindi lakini safari hii nitamchapa na kumaliza ubishi.

“Kama kweli Cheka ni bingwa basi anipige na mimi.”

Kwa upande wa Cheka alisema kuwa yeye ndiye kiboko ya mabondia wa Tanzania, kwa hiyo atammaliza Kaseba kesho ili iwe fundisho.

“Sasa hivi nataka mabondia wa kimataifa, niletewe mabondia kutoka nje. Tatizo hawa hata nikiwapiga hawakomi, wanaendelea tu kung’ang’ania.”

 
Friday, 06 July 2012 08:11 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Kocha Yanga aanza kazi rasmi

Siku moja baada ya kutua Jangwani, kocha mkuu mpya wa Yanga, Tom Saintfiet ameanza kazi kwa kuonyesha kuwa anawajua vizuri kiungo, Haruna Niyonzima na beki, Stephano Mwasyika huku akijinadi kuwa anahitaji makombe yote ambayo timu yake itashiriki.

Saintfiet raia wa Ubelgiji alitua mazoezini kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wakati wa utambulisho alionyesha kuwajua zaidi wachezaji hao kwa kutoa taarifa ambazo zinawahusu.

Mara baada ya Niyonzima kujitambulisha mbele ya kocha huyo alimwambia: “Wewe ndiye ambaye unajua kuzungumza Kifaransa eeh!” Niyonzima akajibu: “Ndiyo.” Wakati kwa Mwasyika alimuuliza: “Nina taarifa zako, wewe si ndiyo ulimpiga refa?”

Swali hilo llisababisha vicheko kutoka kwa wachezaji wengine na ndipo beki huyo aliyekuwa amesimama, alikaa chini bila kujibu chochote huku akitabasamu, likionekana ni swali lililozua mshituko kutokana na kocha huyo mgeni kujua tukio la Mwasyika kumpiga mwamuzi, Israel Nkongo, msimu uliopita.

Utambulisho huo ulipomalizika, Kocha Msaidizi wa Yanga, Felix Minziro alipanga timu iliyocheza dhidi ya Shein Rangers ya Sinza na kupata ushindi wa mabao 5-1. Saintfiet alisema: “Nimefurahishwa na viwango vya wachezaji na nitashirikiana vema na Minziro, kuandaa timu.”

Kuhusu Simba, alisema: “Naifahamu Simba muda mrefu, siwafikirii kabisa kwa sasa na sitaki kuwazungumzia kwa kuwa naelekeza nguvu kwenye kikosi changu.”

Aidha, alisema anawahitaji mazoezini wachezaji wa timu hiyo walio katika kikosi cha taifa chini ya miaka 20, Serengeti Boys, ambao ni Omega Seme, Frank Domayo na Simon Msuva ili kuona viwango vyao.

Katika hatua nyingine ‘injini’ ya usajili ya Yanga, Seif Magari ameliambia Championi Ijumaa kuwa jana saa saba mchana kocha huyo alitarajia kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha timu hiyo.

 
Friday, 06 July 2012 08:06 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Ndege chupuchupu kumtoa roho Thomas Ulimwengu

Nyota wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu jana alinusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea nchini DR Congo.

Ulimwengu raia wa Tanzania anayekipiga TP Mazembe alinusurika katika ajali hiyo akiwa katika ndege iliyokuwa inajaribu kuruka lakini ikashindwa.

Kutokana na kushindwa kupaa, ndege hiyo iliacha njia na kuingia vichakani, Ulimwengu akiwa ndani pamoja na wachezaji wengine 15 wa TP Mazembe na timu ya benchi la ufundi.

Taarifa za ajali hiyo jana zilipatikana saa 8 mchana kupitia katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook wa Ulimwengu, yeye mwenye aliweka maneno haya:

“Dakika chache zilizopita kungeongelewa mambo mengine, labda ningeitwa marehemu au ningekuwa hospitali. Niko ndani ya ndege mimi na wachezaji kama kumi na tano na viongozi na makocha. Ndege imeacha njia na kuingia vichakani, ni baada ya kushindwa kupaa. Mungu mkubwa.”

Baada ya maneno hayo ya Ulimwengu, watu kadhaa walikuwa wakimpa pole mfululizo huku wakimuombea afya njema.

Hata hivyo, Ulimwengu hakuweza kujibu maswali mengi kama ndege hiyo ilikuwa inatokea wapi kwenda wapi na kama alikuwa pamoja mchezaji Mtanzania Mbwana Samatta.

 
Friday, 06 July 2012 07:57 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Okwi azitikisa Simba, Yanga

“BADO Okwi! Bado Okwii! Bado Okwii!” Hivyo ndivyo walivyokuwa wakiimba mashabiki wa Yanga wakati wa mapokezi ya kocha wao mpya Mbelgiji, Tom Saintfiet kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, juzi.

Mashabiki hao walikuwa wakitoa msisitizo huo baada ya kuwepo na taarifa za Yanga kumsajili Emmanuel Okwi wa Simba, kitendo ambacho kimewakera vibopa wa Simba ambao sasa wameamua litakalokuwa na liwe, kwanza ni kumzuia Okwi kisha kuvuruga usajili wa beki Kelvin Yondani aliyetua Jangwani.

Uamuzi wa kuvuruga usajili wa Yondani umefikiwa baada ya vibopa hao wa Simba kubaini kuwa Yanga wanataka kuwafanyia mchezo mchafu, ambapo awali waliamua kuwa wastaarabu kwa kutaka kumruhusu lakini baada ya kuona wanamwitaji na Okwi, sasa wametenga dola 30,000 (Sh milioni 48) kwa ajili ya kazi hiyo.

Chanzo cha habari kutoka Simba kimesema: “Matajiri wa Simba wakiongozwa na Hanspop ambao wapo Zanzibar ilipo timu wamesema watazungumza na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kufanya mipango ya kumbakisha Okwi na kukataa ombi la Yanga kumsajili Yondani.

“Wamekasirika sana na wanadai kuwa lazima wavuruge usajili wa Yondani, ambapo kama TFF ikipitisha beki huyo achezea Yanga, basi wao wamepanga kwenda kukata rufaa Fifa kwa kuwapa viongozi ada ya kukatia rufaa hiyo.”

Wakati huohuo, mashabiki na wanachama wa Simba walifika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Msimbazi wakitaka kujua hatima ya Okwi, wadau hao walimzunguka msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga na kumbana kwa maswali huku baadhi yao wakizungumza kwa jazba kiasi cha Kamwaga kushindwa kujieleza.

 
Friday, 06 July 2012 06:34 Deiwaka World News - Sports News
Print PDF

Cheka atamba kumchakaza Kaseba

Homa ya pambano la ndondi kati ya mabondia wenye majina makubwa nchini, Francis Cheka na Japhet Kaseba, imezidi kushika moto mkali.

Wakati kila mtu akisubiri pambano hilo, Cheka ‘SMG’ ametamba leo kuwa atamfanya kitu mbaya Kaseba katika pambano lao la raundi nane, litakalofanyika Jumamosi ijayo kwenye Tamasha la Usiku wa Tumaini.

Tamasha hilo, litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, likipambwa na michezo pamoja na burudani za aina mbalimbali.

“Mimi ndiyo kiboko ya mabondia wa Tanzania, nitapigana na kumpiga Kaseba kama ambavyo nimeahidi,” alisema Cheka.

Mbali na pambano hilo, siku hiyo kutakuwa na mchezo mwingine wa ndondi katika ya warembo mastaa wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper.

Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo kwenye hoteli ya kisasa ya The Atriums jijini Dar, Wolper alitamba kumpiga vibaya mpinzani wake siku ya Jumamosi kwenye Tamasha la Matumaini pale Uwanja wa Taifa.

“Sipendi maneno, napenda vitendo, nimekuwa nikisikia Wema na rafiki yake wanaongea sana kuhusu mimi kwenye TV.

“Nataka nikate mdomo wake siku hiyo kwa kumpiga,” alisema Wolper.

 

Page 10 of 26

<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>