Music | Lifestyle+Fashion | Antivirus | Love+Relationships | Business+Politics | Sport | TUMA Registrations

You are here:   HomeLifestyle+Fashion
| + -

Lifestyle+Fashion

Friday, 03 May 2013 06:21 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Mbwa ndiye faraja pekee ya Wema kwa sasa

Miss Tanzania 2006-2007, Wema Sepetu amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kwa sasa kama mbwa wake, Ivan na Gucci.

Wema alisema hawezi kukaa zaidi ya siku tatu bila kuwaona mbwa wake hao kwani amewazoea kwa kuwa humuondolea ‘stress’ za hapa na pale.

“Juzikati nilikwenda Arusha mara moja tu siku hiyohiyo nikawa nawakumbuka Ivan na Gucci mpaka nikawa natamani kurudi kwa ajili yao, kusema kweli hawa ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Wema na kuongeza:

“Nimewazoea lakini wao pia ndiyo zaidi, hawataki kubanduka pindi ninaporudi kutoka katika kazi zangu, mtu akiwachukua tu umewakorofisha.”

 
Wednesday, 24 April 2013 19:19 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Miss Utalii sasa kimeeleweka

Baada ya Kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 ambayo imeanza upya kwa kasi ya ajabu ambapo wadau mbali mbali ikiwa ni asasi za Serikali, Taasisi mbalimbali, Makampuni pamoja na watu mbalimbali wamejitokeza kudhamini Fainali Hizo za Miss Utalii Tanzania Taifa Ambazo zitafanyika Mwanzoni mwa Mwezi Ujao.

Walio jitokeza Kudhamini ni pamoja na. TANAPA, Ngorongoro Crater, Tanzania Tourist Board, Mtwana Catering, Ikondolelo Lodge Hotel, Sahara Media Group, Mbasha Entertainment, Sophia Records,Nyinda Hotel, Tanga Beach Resort, Retco, Tanzania School of Journalism and Mass Communication,  Oriental Berau De Change, Clouds Media Group, Times FM, Global Publishers, Tone Multimedia Group, Dar es salaam City College, Eden Hill College, Maweni Hotel.

Bado kuna wadau wengine mbalimbali ambao wanaendelea kujitokeza kwa ajili ya Kudhamini Fainali Hizo za Miss Utalii Tanzania 2012/13.

Mpaka sasa Kambi mpya ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 ipo na inaendelea Vizuri, Warembo zaidi ya 30 wamejiandaa vizuri  kwa ajili ya Fainali Hizo zitakazo fanyika Mwanzoni mwa mwezi Ujao ikiwa ni pamoja na Kutoka Mikoa yote Tanzania, Kanda Maalum ya Zanzibar na Vyuo vikuu Tanzania.

Washindi wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism University World, Miss Globe International n.k

Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World 2007-Africa, Miss Tourism Model Of The World 2008-Personality n.k

 
Thursday, 18 April 2013 06:22 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Wastara wa Sajuki apata pigo lingine

NI pigo juu ya pigo kwa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ambaye miezi minne iliyopita alifiwa na mumewe, Juma Juma Kiwoloko na sasa amepatwa na msiba mwingine mkubwa.

Msiba huu wa sasa umemfanya Wastara kulazwa jijini Dubai baada ya kupata mshtuko kufuatia mdogo wake wa kiume, Abdulmalik  kupigwa risasi na kufariki dunia jijini Dar.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa manane, kuamkia Aprili 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Lango la Jiji Magomeni Mikumi wakati Abdulmalik alipokuwa akiamua ugomvi kati ya dada yake aitwaye Hawa na shemeji yake aliyejulikana kwa jina la mzee Lyimo.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu aitwaye Nuru, marehemu siku ya tukio alikuwa nyumbani kwao Magomeni Mikumi na  ilipotimu saa sita usiku alipigiwa simu na Hawa akimuomba aende kumchukua katika Ukumbi wa Lango la Jiji ili warudi nyumbani.

“Wakiwa katika ukumbi huo, muda mfupi baadaye alitokea mzee Lyimo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na Hawa na kuanza kumvamia na kumpiga mwanamke huyo.”

Nuru alisema kuwa kipigo hicho kiliwashtua watu wengi waliokuwa katika eneo hilo na kumfanya Abdulmalik kuingilia ili kuamua ugomvi huo na kumuokoa dada yake asiendelee kupigwa.

“Baada ya kuona hivyo, mzee Lyimo alichomoa bastola na kupiga hewani kuwatawanya watu, wakati Abdulmalik alipokuwa akiamua risasi moja ikampata tumboni,” alisema Nuru kwa masikitiko.

Nuru alidai kwamba baada ya Abdulmalik kupigwa risasi, alipatwa na kiwewe na kuanza kukimbia hadi nyumbani, kisha akajifungia ndani, baadaye akamwambia kaka yake mwingine kwamba alipigwa risasi ya tumboni na shemeji yao.

Binti huyo aliendelea kusema kwamba wakati ndugu hao wakijadiliana, mzee Lyimo alifika nyumbani hapo na kumchukua Abdulmalik kisha kumpeleka katika Hospitali ya Mikumi. Alipomfikisha, alitoweka na kumuacha kijana huyo hospitali hapo.

“Kwa kweli alikuwa katika hali mbaya, ndugu tukaamua kumpeleka Muhimbili lakini tukiwa njiani, Abdulmalik alifariki dunia,” alisema Nuru na kuanza kulia.

Dada huyo alisema kuwa madaktari wa Hospitali ya Mikumi katika uchunguzi wao walibaini kwamba risasi iliyokuwa imempata Abdulmalik ilikuwa imepanda kutoka tumboni na kufika kifuani.

“Yaani kiukweli kifo cha kaka Abdulmalik kinaumiza, ndugu hawaamini na hatujui hali ya Wastara ambaye amelazwa baada ya kupatwa na mshtuko pale tulipompa habari hizi,” alisema Nuru.

Ripota wetu alijaribu kuwasiliana na Wastara kwa njia ya simu, hata hivyo staa huyo alisema kuwa alikuwa katika hali mbaya kutokana na msiba huo na kulazwa kwa mapumziko hivyo asingeweza kuongea vizuri mpaka atakapokuwa sawa.

“Siwezi kwa kweli… naomba niache, nimelazwa kwa mapumziko…” alisema kwa sauti iliyoonesha kwamba alikuwa akilia.

 

 
Tuesday, 09 April 2013 06:20 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Irene Paul: Nitazidi kumlilia Kanumba

Irene Paul, msanii aliyeigiza kumsukuma Kanumba akaanguka na kufa kwenye filamu ya Power & Love kama ilivyotokea kwenye kifo cha kweli, amesema aataendelea kumlilia staa huyo, aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu.

Akichonga na ripota wetu juzikati Dar, Irene alisema awali alikuwa hatamani kuitazama filamu hiyo itakayoingia mitaani Aprili 12, mwaka huu kupitia Kampuni ya Steps Entertainment lakini kwa sasa anasubiri kulia tena.

“Nilitaka nisiitazame Power and Love, lakini sina jinsi, najua nitaiona, hapa najiandaa kulia tena kama ilivyokuwa kwenye kifo chake na najua nitazidi kumlilia kila nitakapokuwa naiona hiyo filamu,” alisema Irene.

 
Friday, 03 May 2013 05:47 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Mastaa wa Bongo, pete nyingi ndoa sifuri

Katika ulimwengu huu kuna mambo mengi yanayofurahisha. Yapo pia yanayosikitisha na utapeli katika uhusiano wa kimapenzi umetamalaki.

Utangulizi huo una maana kuwa katika jamii inayotuzunguka inabidi mtu uwe makini la ivyo utajikuta kwenye wakati mgumu hasa kwa wasichana wanaohitaji kuolewa.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuwarubuni wanawake wakiwadanganya kuwa watawaoa, ahadi ambazo hazitimii kwani mapenzi yao huwa yanaishia njiani kabla hawajatimiza lengo na kuwaacha wenzao katika maumivu makali.

Katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, ishu hiyo ndipo nyumbani kwao ambapo leo katika makala haya tutaona orodha ya wasanii ambao wamevishwa pete za uchumba lakini suala la ndoa limeishia ndotoni.

Ni kama wanaota lakini wakiamka hujikuta wakijuta kuwa walikosea wapi. Kinachoonekana kwa sasa ni kwamba pete ya uchumba ni ndoano ya kumnasa mwanamke na baada ya kukidhi matwakwa humwacha bila kutimiza ahadi ya ndoa.

FLORA FESTO MVUNGI

Ni mwigizaji wa filamu za Kibongo anayeishi kinyumba na mwanamuzki wa Kizazi Kipya, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba’.

Tangu Flora avishwe pete ya uchumba na H. Baba pamoja na kutolewa mahari, siku zimesonga bila kuona suala la ndoa likiendelea.

Wasanii hawa kila wakiulizwa kuhusu suala la ndoa huwa wanajibu hivi karibuni ambapo kwa sasa kuna madai kuwa tayari Flora ana ‘kibendi’.

ROSE DONATUS NDAUKA

Ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo ambaye alichumbiwa kwa muda mrefu na jamaa aliyekuwa mmoja wa kundi la kitambo la Bongo Fleva kutoka Tanga la TNG, Malick Bandawe.

Rose amekuwa akiahidi kila kukicha kuwa harusi yake iko mbioni lakini umepita muda mrefu hakuna ndoa wala nini na badala yake wamebaki kuishi pamoja kama mume na mke.

OTILIA BONIFACE

Ni mkata mayenu kiraka wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’. Alivishwa pete ya uchumba miaka miwili iliyopita na mume wa mtu anayejulikana kwa jina moja la Ally lakini mpaka sasa ndoa imebaki ndotoni.

Otilia na mchumba wake huyo wanaishi pamoja kama mume na mke na suala la ndoa bado wanajiandaa.

SUZAN CHUBWA ‘QUEEN SUZY’

Ni mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’. Alivishwa pete ya uchumba zaidi ya miaka miwili iliyopita na aliyekuwa rapa wa bendi hiyo, Aimerichard Mwamba ‘G-Seven’ ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake Nairobi, Kenya na kumwacha Suzy Bongo.

G-Seven alimposa Suzy pamoja na kumvisha pete ambapo uchumba wao ulidumu kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni bishosti huyo kuweka wazi kuwa ameamua kuachana naye kwa sababu aligundua kuwa siyo mwaminifu.

ISABELA MPANDA

Ni Miss Ruvuma 2006. Anasaka mkate wa siku kupitia filamu na muziki wa Bongo Fleva. Alivishwa pete ya uchumba kitambo na kutolewa mahari na mwanaume jina kapuni lakini aliishia kupewa mimba na kuzaa.

Baada ya kuzaa Isabela mpaka sasa hajaolewa na amejaliwa kuwa na watoto wawili kila mmoja na baba yake huku ikifahamika kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Luteni Kalama.

MIRIAMU GERALD

Ni Miss Tanzania 2009 aliyevishwa pete ya uchumba na msanii wa filamu za Kibongo, Kennedy Victor ‘Kenny’. Walipanga kufunga pingu za maisha mwezi Juni, mwaka jana lakini hadi unaposoma hapa hakuna chochote zaidi kujaliwa mtoto mmoja wa kiume.

WEMA SEPETU

Ni mwanadada mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo. alivishwa pete ya uchumba na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mapenzi yao hayakufika mbali, waliishia kuachana na mambo ya ndoa yakaishia hapo huku bidada akiendelea kujikusanyia pete za uchumba kabatini kwake baada ya ile ya Yusuf Jumbe.

SHAMSA FORD

Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye kwa muda mrefu amechumbiwa na jamaa mmoja aitwaye Dick. Uchumba wao una zaidi ya miaka miwili lakini ndoa imekuwa ni kitendawili huku wakijaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry.

SALMA JABU ‘NISHA’

Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye aliwahi kudaiwa kuvishwa pete ya uchumba na mwigizaji mwenzake aitwaye Godfrey Kusila kabla ya uchumba kuvunjika na penzi kuhamia kwa mwanamuziki Elibariki Emmanuel ‘Ney wa Mitego’. Hata hivyo, kwa Ney wa Mitego napo uchumba uliota mbawa pamoja na kuwa na mbwembwe nyingi.

 
Tuesday, 23 April 2013 14:42 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Wema akata tamaa ya maisha

Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu, amekata tamaa ya maisha kufuatia matukio mfululizo yanayomuandama.

Wema, kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, aliandika kuwa anaamini atakufa na kuacha maneno mengi ya kumuongelea kwa mazuri.

Kuhusu kile ambacho Wema amekisema, soma ujumbe huo katika picha kama ulivyonakiliwa kwenye akaunti yake ya Instagrama.

 
Thursday, 11 April 2013 11:07 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Beckham adaiwa kukuza nyeti

Kiungo wa PSG, David Beckham, amedaiwa kuchoma sindano ya kukuza maulile yake nyeti ili awe mkali zaidi kunako uwanja wa faragha.

Kwa mujibu wa gazeti moja la England, Beckham ‘alibusti’ nyeti zake kwa sindano, lengo kupata mwonekano mzuri hata anapovaa nguo za ndani ya boxer.

“Kila kitu kuhusu Beckham na alichofanya kukuza ukubwa wa nyeti zake, kinajulikana,” kilisema chanzo cha habari. “Kwa kipindi hiki anavaa boxer kwa ajili matangazo, namna anavyoonekana sasa akiwa na boxer, ndivyo alitaka na sasa imekuwa.”

Inadaiwa kuwa kiungo huyo mwenye heshima kubwa England, aliwahi kushauriwa kufanya upasuaji lakini mwenyewe aligoma na akataka achomwe sindano, kitu ambacho kilifanyika.

Imebainishwa kuwa Beckham anakuwa mmoja wa wanaume wa England na Uingereza yote kwa jumla ambao wamefanya mambo mbalimbali kuhakikisha wanakuza nyeti zao.

Inazidi kuelezwa kuwa wanaume wa Uingereza, wapo radhi kutoa fedha nyingi ili wafanyiwe upasuaji au kuchomwa sindano waweze kukuzwa nyeti zao kwa imani kuwa zinawaongezea mvuto wa kimapenzi kwa wanawake.

“Itabidi uchunguzi ufanyike, ni kwa nini sasa hivi wanawake wengi wa Uingereza wawe wanataka sana maumbo makubwa ya nyeti za wanaume. Huko nyuma hakukuwa na hisia hizi, kila mmoja aliridhika na umbile lake lakini sasa ni shughuli,” alisema.

 
Tuesday, 02 April 2013 21:04 Al News - Lifestyle+Fashion
Print PDF

Afya ya Lulu yatia shaka

Wiki kadhaa baada ya kuachiwa kwa dhamana, afya ya mkali wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ inadaiwa kutia shaka kwani amepungua uzito wa kilo kumi.

Jumatatu wiki iliyopita, Lulu aliwashtua askari magereza alipofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya mwigizaji mwenzake, Kajala Masanja waliokaa wote ndani ya nondo za mahabusu ya Gereza la Segerea.

Akiwa mahakamani hapo, baadhi ya askari hao waliokuwa wakimlinda staa huyo alipokuwa Segerea wakimshuhudia akiwa amenenepeana, walionekana wakimshangaa na kuulizana kulikoni amekonda ghafla.

Ripota wetu alimbana Lulu kuhusu ishu hiyo na akafunguka kuwa kwa sasa anafanya mazoezi na amefanikiwa kupungua kilo kumi.

Alisema alipokuwa selo alikuwa amenenepa hadi kufikia uzito wa kilo 69 lakini baada ya mazoezi mazito anayofanya amepungua hadi kilo 59 kitendo ambacho kimewafanya watu wamshangae.

Alisema daktari alimuonya vikali juu ya unene aliokuwa nao hivyo akakubali kufuata masharti ya kupunguza mwili, jambo ambalo limempa mtihani mwingine wa watu kutia shaka afya yake.

Lulu alikaa gerezani Segerea maarufu kwa jina la kistaa la Segedansi kwa takribani miezi kumi akikamiliwa na shitaka la kuua bila kukusudia akihusishwa na kifo cha Steven Kanumba ambapo kesi inasubiria kuanza kuunguruma.

 

Page 1 of 33

<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>